Loading...

Mario Baloteli afanyiwa vitendo vya ubaguzi nchini Ufaransa

Mario Balloteli ni mmoja kati ya wachezaji wakorofi na wasioisha vituko uwanjani. Hakuwa na wakati mzuri alipokuwa Uingereza. Man City alifanya matukio mengi ikiwemo kukunjana na kocha wake Roberto Mancini baadae akajiunga na Liverpool ambal walimuuza Ufaransa,akiwa Nice anaonekana kuanza kurudi katika fomu yake.

Ijumaa iliyopita timu yake ya Nice ilitoka sare dhidi ya Bastia. Lakini Baloteli katika mechi aliitwa nyani na shabiki wa Bastia. Kupitia ukurasa wake wa instagram Balloteli aliandika “matokeo ya jana yalikuwa sawa na refa alikuwa mzuri.”

“Lakini nataka kuwauliza watu wa Ufaransa ,hivi ni sawa mashabiki wa Bastia kupiga kelele za nyani mechi nzima halafu hakuna yeyote anayeliongelea hili?kwa Ufaransa ubaguzi ni jambo la kawaida au hii ni kwa Bastia tu?aibu kubwa”

Lakini Bastia hawakukaa kimya walimjibu Baloteli,katika taarifa waliyotoa walisema hawajapewa taarifa kutoka sehemu yoyote kwamba kulitokea tukio kama hilo.Waliongeza kwa kuonya kwamba taarifa za namna hiyo zinaichafua timu yao.

Kamati inayohusiana na masuala ya nidhamu Ufaransa ilisema kuanzia Alhamisi watafungua faili linalohusiana na suala hilo. Kamati hiyo pia itachunguza suala la basi la timu ya Nice kushambuliwa na mawe kabla ya mechi hiyo.

Hii sio mara ya kwamza kwa Baloteli kupitia masuala ya ubaguzi wa rangi,kwani msimu wa mwaka 2014/2015 Balloteli alipokea uhumbe kuhusu kumbagua mara 4000 kupitia mitandao ya kijamii.

ZeroDegree.
Mario Baloteli afanyiwa vitendo vya ubaguzi nchini Ufaransa Mario Baloteli afanyiwa vitendo vya ubaguzi nchini Ufaransa Reviewed by Zero Degree on 1/23/2017 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.