Loading...

Marufuku kufanya biashara ya silaha za jadi pembezoni mwa barabara

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro 
Jeshi la polisi limepiga marufuku uuzaji wa silaha za jadi kama panga, mishale, manati, visu pembezoni mwa barabara nyakati za foleni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kumekuwa na vitendo vya kiarifu vikifanyika kwa baadhi ya wafanyabiashara hao pia ni hatari kwa hali ya usalama wa wananchi. 

“Biashara hii imeshamiri kwa kasi katika barabara ya Nyerere, Tazara na kwenye mataa ya Chang’ombe na Gerezani huwa wanawaibia watu kwenye magari binafsi na umma vitu kama pochi, kompyuta mpakato, saa na simu za mikononi,” amesema Sirro.

Sirro amesema tayari jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja na Mgoli S/O Sakalani (39) mkazi wa Banana, Ilala na mtu yoyote atakayetaka kufanya biashara hiyo ni lazima kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo na anatakiwa kuwa na eneo maaulum litakalotambulika kisheria.

ZeroDegree.
Marufuku kufanya biashara ya silaha za jadi pembezoni mwa barabara Marufuku kufanya biashara ya silaha za jadi pembezoni mwa barabara Reviewed by Zero Degree on 1/13/2017 05:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.