Loading...

Migogoro Anglicana ni ya Kupandikizwa, Askofu Mokiwa.

Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, amesema migogoro mingi inayotokea katika kanisa hilo ni ya kutengenezwa jambo linalowavunja mioyo waumini.

“Kanisa ndilo kimbilio la waumini wenye shida mbalimbali, sasa kukiwa na migogoro waumini watamkimbilia nani?” alisema 

Dk Mokiwa alizungumza hayo jana na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni ambapo Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican nchini, Jacob Chimeledya alimtaka Dk Mokiwa ajiuzulu.

Askofu Chimeledya alimtaka Askofu Mokiwa ajiuzulu kwa kile alichodai kuwa anatumia madaraka yake vibaya na ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, katika kikao chake na wanahabari leo asubuhi, Askofu Mokiwa alikanusha na kudai kuwa migogoro hiyo inapandikizwa na maadui zake.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Migogoro Anglicana ni ya Kupandikizwa, Askofu Mokiwa. Migogoro Anglicana ni ya Kupandikizwa, Askofu Mokiwa. Reviewed by Zero Degree on 1/10/2017 05:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.