Loading...

Huyu ndiye aliyetwaa tuzo ya FIFA ya kocha bora duniani kwa mwaka 2016

Ilikuwa ni lazima apatikane mshindi mmoja tu. Claudio Ranieri ndiye aliyetajwa kama kocha bora duniani kwa mwaka 2016 katika tuzo za FIFA siku ya Jumatatu.

Ranieri, mwenye umri wa miaka 65, aliiongozwa Leicester City kupata mafaniko makubwa katika historia ya soka kwa kubeba taji la ligi msimu wa 2015-16 kwa kuzidondosha chini timu zote kwa mtindo wa kushangaza. Kutoka kuipandisha daraja timu na kuipatia taji.

Kweli ilikuwa moja matukio
 katika historia ya soka yaliyoshangaza wengi na kuacha mashabiki wengi wa soka duniani kote wakiduwaa.

Akipokea tuzo yake kutoka kwa nyota wa zamani wa Argentina, Diego Maradona Zurich, nchini Uswisi siku ya jana Jumatatu, Ranieri alikuwa kama haamini vile na kusema haya huku akiwa na furaha nyingi.



"Kushinda tuzo hii tu, mimi najihisi kama kichaa hadi sasa. Nawashukuru sana wale wote ambao walinipigia kura. Nataka kuwashukuru familia yangu, mke wangu, wakala wangu, mwenyekiti wangu na wachezaji wangu, "Ranieri alisema. "Nadhani kile kilichotokea msimu uliopita kilikuwa cha ajabu kweli. Ilikuwa ni kitu cha ajabu kwa sababu miungu ya soka ilisema 'Leicester lazima ishinde. Hivyo tu, hivyo tu! ' "

Ranieri alifanikiwa kuwagaragaza chini kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na wa Ureno Fernando Santos katika tuzo hii.


ZeroDegree.
Huyu ndiye aliyetwaa tuzo ya FIFA ya kocha bora duniani kwa mwaka 2016 Huyu ndiye aliyetwaa tuzo ya FIFA ya kocha bora duniani kwa mwaka 2016 Reviewed by Zero Degree on 1/10/2017 05:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.