Loading...

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco atumbuliwa.



Taarifa kutoka Ikulu
Rais John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felschemi Mramba kuanzia leo, Januari 1, 2017.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kuwa kaimu mkurugenzi wa shirika hilo. Kabla ya uteuzi huo, Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

ZeroDegree.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco atumbuliwa. Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco atumbuliwa. Reviewed by Zero Degree on 1/01/2017 05:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.