Loading...

VIDEO: Rais Magufuli akataa kupanda kwa bei ya umeme.

Rais John Magufuli amesema licha ya Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati maji (Ewura) kuridhia ombi la Tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzia Januari Mosi, 2017 bei ya umeme haitapanda.

Rais Magufuli amezungumza hayo leo katika Kanisa Kuu Katoliki la Bukoba aliposali wakati wa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kagera.

Rais ameshangazwa na kitendo cha watendaji waliopandisha bei ya umeme bila hata ya kushauriana na yeye, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.




''Ninamshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini kwa maamuzi ya kusitisha hayo. Kwa hiyo umeme hakuna kupanda bei, Amesema.


Ameongeza kuwa, “Haiwezekani unapanga mikakati ya kujenga viwanda na hasa katika mikakati mikubwa ya nchi ya kusambaza umeme mpaka vijijini kwa watu maskini halafu mtu mmoja kwa sababu ya cheo chake anapandisha bei, hili haliwezekani.''

ZeroDegree.

VIDEO: Rais Magufuli akataa kupanda kwa bei ya umeme. VIDEO: Rais Magufuli akataa kupanda kwa bei ya umeme. Reviewed by Zero Degree on 1/01/2017 05:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.