Loading...

BREAKING News: Mkwasa sio kocha wa taifa stars tena, ..TFF yamtangaza kocha mpya.

Chalres Boniface Mkwassa
Kocha mzawa ambae ameiongoza timu ya taifa kwa muda mrefu Chalres Boniface Mkwassa, sasa hivi sio kocha tena wa timu yetu ya taifa.

Taarifa hivi zimethibitishwa na rais wa TFF ndugu Jamal Malinzi kupitia ukurasa wa twitter. Jamal Malinzi ametoa taarifa hiyo kwa kuandika,“Mkataba wa TFF na Kocha Mkwassa,kwa makubaliano,umefikia mwisho leo.Salum Mayanga ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda wa Taifa Stars.”



Ikumbukwe kamba kocha huyu alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambae alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015.

Endelea kufatilia katika ukurasa huu utajua zaidi kuhusu kusitishwa kwa mkataba huu na sababu zake kama zitawekwa wazi na moja kati ya pande hizi mbili.


ZeroDegree.
BREAKING News: Mkwasa sio kocha wa taifa stars tena, ..TFF yamtangaza kocha mpya. BREAKING News: Mkwasa sio kocha wa taifa stars tena, ..TFF yamtangaza kocha mpya. Reviewed by Zero Degree on 1/02/2017 08:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.