Loading...

Msuva avujisha siri za Yanga.

WINGA wa Yanga, Simon Msuva, amesema ubunifu na kupenda kujifunza ndiyo siri kubwa ya yeye kupachika mabao katika michezo mbalimbali ya timu hiyo ya Jangwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msuva alisema kutokana na kasi aliyonayo kamwe hatabweteka isipokuwa amejipanga kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo Jangwani katika michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Najua mengi yamezungukwa na pia nimesoma katika magazeti lakini hiyo haitoshi kunifanya nibweteke mimi nafanya kazi kwa ajili ya timu yangu hayo mengine wataamua wao mimi sina la kusema,” alisema Msuva.

Winga huyo aliongeza kuwa katika suala zima la upachikaji wa mabao msimu huu amekuwa na wakati mzuri zaidi kutokana na kuwa mbunifu katika suala zima la kujipanga akiwa uwanjani.

“Nimekuwa nikifunga sana mabao lakini naweza kusema msimu huu nimekuwa mbunifu zaidi kutokana nawasoma mabeki wa timu pinzani halafu nakuwa mbunifu katika kuwaibia ndio maana utakuta wananisahau na kuwafunga,” aliongeza Msuva.

Msuva aliongeza kuwa kitu kingine kinachomfanya kuendelea kuzitesa nyavu za timu pinzani ni kutokana na yeye kupenda kujifunza mbinu mbalimbali ikiwemo kufanya mazoezi yake ya ziada.

“Nimekuwa na programu zangu pekee nikimaliza programu ya pamoja napenda sana kujifunza mbinu za kufunga ndio maana utaona kila siku nazidi kuwa mtamu,” aliongeza.

Mpaka sasa winga huyo ameshapachika wavuni mabo manne katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Unguja na kumfanya kuongoza orodha ya wafungaji.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Msuva avujisha siri za Yanga. Msuva avujisha siri za Yanga. Reviewed by Zero Degree on 1/07/2017 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.