Loading...

Nini kimemsibu Kichuya?


UKAME wa mabao umewaandama washambuliaji watatu wa Simba na Yanga, huku ikibainika kwamba Shiza Kichuya hajapachika bao lolote tangu kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina asaini mkataba na kuanza kazi rasmi.

Kichuya ambaye ni mwenyeji wa Morogoro mwenye mabao tisa akiwa sawa na wafungaji wawili wa Yanga, Amissi Tambwe na Simon Msuva,winga huyo alifunga mara ya mwisho Novemba 2 mwaka jana katika mchezo dhidi ya Stand United akifunga bao pekee la ushindi katika mechi iliyomalizika kwa bao 1-0 akifunga kwa penalti.

Tangu afunge bao hilo matukio kadhaa yamechukua nafasi likiwemo la mwaka kubadilika lakini pia Lwandamina aliyewasili nchini Oktoba 24 kuanza kazi Jangwani. Lwandamina alisaini Yanga Novemba 10 na kuanza kazi siku 18 baadaye, lakini hali mbaya zaidi ni kwa mshambuliaji Laudit Mavugo wa Simba aliyefunga bao la mwisho Oktoba 23 ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasili kwa Lwandamina.

Mavugo alifunga bao la mwisho Oktoba 23 wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto African ya Mwanza mchezo uliopigwa jijini Dar es Salaam. Yanga nako aliyekumbwa na ukame wa namna hiyo ni Mzambia Obrey Chirwa mwenye mabao matano ambapo alifunga bao lake la mwisho Oktoba 26 wakati akiifungia Yanga bao la kuongoza wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu.

Chirwa baada ya kufunga bao hilo dunia imeshuhudia matukio kadhaa yakijiri yakiwemo nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard akistaafu soka rasmi uamuzi aliotangaza Novemba 24 pia hivi karibuni makocha wote wa Azam kutoka Hispania walitimuliwa kazi.

BABA WA KICHUYA AIBUKA
Baba wa Kichuya, Mzee Ramadhan Kichuya ametaja sababu mbili: ‘‘Nimeona mambo mawili kwa mwanangu, maana mkubwa ni mkubwa tu. Kichuya alianza vizuri sana alipotua Simba na si kwamba anafanya vibaya sasa hivi, ila alijisahau na kubweteka alipokuwa anafunga mara kwa mara, jambo ambalo nimekuwa nikizungumza naye mara nyingi kuwa ukibweteka kuna wenzako wanakuja nyuma yako.”

“Kubweteka kwake ndiko kumesababisha wenzake wamfikie kwenye ufungaji wa mabao ila akijirekebisha na kujitambua basi atafunga zaidi ingawa sasa wenzake wameanza kuonekana bora zaidi, Mzamiru ndiye anajua kumtengenezea mipira Kichuya ili afunge ingawa na yeye siku hizi anataka kufunga, hivyo anakosa mtu wa kumchezesha,” alisema Mzee Kichuya.

Source: Mwnanspoti
ZeroDegree.
Nini kimemsibu Kichuya? Nini kimemsibu Kichuya? Reviewed by Zero Degree on 1/07/2017 11:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.