Loading...

Payet ashtukia mpango wa West ham

Dirisha dogo la usajili la Januari linakaribia kufungwa na mambo yakiwa bado ni magumu kwa kiungo wa West Ham United, Dimitri Payet ambaye tangu msimu wa 2016/2017 kuanza amekuwa akiushinikiza uongozi wa klabu hiyo kumuuza ili aondoke klabuni hapo.

Payet aliamua kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu lakini kuonekana kugonga mwamba na kuamua kufikia uamuzi wa kugoma kucheza katika kikosi cha timu hiyo na kwenda kufanya mazoezi na timu ya vijana chini ya miaka 23 ili tu kushinikiza uongozi umwachie na bado hali inaonekana kuwa ni ngumu kwa uongozi wa klabu hiyo kumruhusu.

Baada ya mbinu zote za kuzungumza na uongozi na kugoma kuchezea timu ya wakubwa kuonekana kushindikana, Payet sasa amemua kugomea na mazoezi ya timu ya vijana ili kuwashawishi viongozi wa timu hiyo kumwachia aondoke kabla ya dirisha dogo kufungwa.

Awali kocha wa Kocha wa Wes Ham, Slaven Bilic alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa timu hiyo ipo tayari kumpa chochote lakini si kumwachia mchezaji muhimu kama yeye kuondoka na watahakikisha kila liwezekanalo kumbakiza mchezaji huyo raia wa Ufaransa ili aitumikie klabu hiyo kwa muda mrefu.

Kwa msimu wa 2016/2017, Payet ameichezea West Ham michezo 18, akifunga magoli mawili na kutoa pasi za magoli sita.

ZeroDegree.
Payet ashtukia mpango wa West ham Payet ashtukia mpango wa West ham Reviewed by Zero Degree on 1/27/2017 05:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.