Loading...

Rais Donald Trump aonywa na Korea Kasikazini

Gazeti la Rodong Sinmun la chama tawala cha Korea Kaskazini limeandika kuwa, nchi hiyo itaendelea kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia na nguvu zake za kiulinzi.

Serikali ya Korea Kaskazini imemuonya Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu siasa zake za kiuhasama na kusema kama nchi hiyo itapanga kuishambulia, Pyongyang itakuwa ya kwanza kuanzisha mashambulizi.

Gazeti la Rodong Sinmun la chama tawala cha Korea Kaskazini limeandika kuwa, nchi hiyo itaendelea kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia na nguvu zake za kiulinzi.

Limefafanua kuwa Pyongyang inatambua kuingia madarakani kwa Rais huyo mpya kumeifanya hali ya mambo kimataifa kuwa mbaya zaidi na ili kukabiliana nayo, haina njia nyingine zaidi ya kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi na silaha za nyuklia.

Kadhalika ripoti hiyo imesisitiza kuwa, Korea Kaskazini kama moja ya nchi zenye uwezo wa nyuklia duniani, inafanya juhudi za kuimarisha usalama na itaendeleza siasa hizo.

Gazeti hilo limekosoa vikali mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka yanayofanywa kwa pamoja na Marekani na Korea Kusini ambayo mwaka huu yamepangwa kufanyika Machi na kusisitiza kuwa, mazoezi hayo yamelitia hatarini eneo zima la Peninsula ya Korea.

ZeroDegree.
Rais Donald Trump aonywa na Korea Kasikazini Rais Donald Trump aonywa na Korea Kasikazini Reviewed by Zero Degree on 1/27/2017 12:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.