Loading...

Shule 3 zafungwa kwa sababu ya kukosa vyoo

Jengo la vyoo vya shule mojawapo lililochakaa hivyo kusababisha kero kwa wanafunzi. 
Shule tatu zenye wanafunzi 3,971 wilayani ukerewe mkoani Mwanza, zimefungwa tangu Januari 13 kwa kukosa vyoo.

Shule hizo na idadi ya wanafunzi kwenye mabano ni Chankaba (1,200), Miti Mirefu (823) na Maregea (1,948). 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe, Frank Bahati alisema tatizo hilo limesababisha walimu 21 kushushwa madaraka kwa kushindwa kushirikiana na jamii ili kulitatua.

Mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji katika Halmshauri ya Ukerewe, Makole Chilato alisema shule hizo zilifungwa kutokana na kukosa vyoo hali iliyohatarisha usalama wa afya zao.

Alisema hivi sasa ujenzi wa vyoo katika shule hizo unaendelea.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati alisema tatizo la vyoo katika shule hizo limesababisha kuwaondoa madarakani walimu 21 kwa kushindwa kutafutia ufumbuzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Ukerewe, Marwa Tuyi alisema alipokea taarifa hiyo kwa mshutuko mkubwa na ameanza kufuatilia ili kujua kama utaratibu, miongozo na sheria zilifuatwa.

Alisema sio wajibu wa walimu kujenga vyoo na miundombinu mingine ya shule, hivyo hakubaliani na hatua zilizochukuliwa dhidi ya walimu hao.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Shule 3 zafungwa kwa sababu ya kukosa vyoo Shule 3 zafungwa kwa sababu ya kukosa vyoo Reviewed by Zero Degree on 1/28/2017 12:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.