Loading...

Siri ya Rais Magufuli kuwapa kipaumbele wasomi wa ndani katika uteuzi wake.

Imeelezwa kuwa siri ya Rais John Magufuli kufanya uteuzi wa Watanzania wataalamu wa ndani badala ya kuchukua wanaofanya kazi nje ya nchi, ni pamoja na msimamo wake wa kutolipa mishahara mikubwa lakini pia kuwatia moyo wasomi waliamua kubaki nyumbani.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, Rais Magufuli ameonekana kuteua wataalamu na wasomi kutoka sekta binafsi na taasisi za umma ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), tofauti na mtangulizi wake Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliyeonekana wakati mwingine akichukua Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi.


Hata hivyo, wachambuzi wameeleza kuwa licha ya Watanzania wote kuwa na haki ya kufanya kazi nchini kwa sifa na vigezo vinavyohitajika, kinachotakiwa kuangaliwa ni uwezo na vipaumbele vya wataalamu wanapopatikana.

Miongoni mwa wachambuzi waliozungumzia mazingira hayo, Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Repoa, Dk Abel Kinyondo aliyesema licha ya muda mfupi ambao amekaa madarakani, ni vyema Rais Magufuli kuchukua tahadhari katika uteuzi wake.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Siri ya Rais Magufuli kuwapa kipaumbele wasomi wa ndani katika uteuzi wake. Siri ya Rais Magufuli kuwapa kipaumbele wasomi wa ndani katika uteuzi wake. Reviewed by Zero Degree on 1/04/2017 11:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.