Loading...

Treni ya abilia iliyopata ajali Mkoani Pwani yaanza safari

Treni ya Deluxe Coach iliyopata ajali jana, imeendelea na safari zake leo (Jumatatu) saa 9 alasiri kuelekea Kigoma na Mwanza baada ya mabahewa yaliyokuwa yamesalia kwenye reli kuondolewa.

Kamanda wa kikosi cha Polisi Reli, Simon Chillery amesema kuwa safari zimeanza baada ya kikosi cha mafundi kifanikiwa kuondoa mabehewa yaliyosalia katika reli, kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta.

“Treni imeondoka leo saa 9 alasiri na inatarajiwa kufika Kigoma Jumatano saa 4 asubuhi, pamoja na hayo uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha ajali ukikamilika tutawapa taarifa,” amesema Chillery.
Treni ya abilia iliyopata ajali Mkoani Pwani yaanza safari Treni ya abilia iliyopata ajali Mkoani Pwani yaanza safari Reviewed by Zero Degree on 1/30/2017 06:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.