Tumia Juisi ya Limao kuondoa madoa ya chunusi usoni
Watu wengi hulalamikia tatizo la kutokwa na chunusi usoni ambazo huharibu kabisa mwonekano wao. Hata hivyo, baada ya mara kadhaa kuwaelekeza njia za kiasili za kuondoa na kupunguza chunusi, wengi wamekuja na tatizo jingine. Baada ya chunusi kupona, huacha makovu ambayo nayo hukera sana na kuharibu mwonekano wa ngozi.
Mahitaji
Tengeneza juisi ya malimao bila kuongeza maji au kitu kingine chochote. Paka usoni na iache ikauke kabisa. Subiri mpaka baada ya dakika thelathini, osha uso wako. Unaweza kutumia pia kitambaa cha pamba kujisugua taratibu kwenye uso wako kisha nawa vizuri.
Unaweza kurudia zoezi hili hata mara mbili kwa siku na endelea mpaka wiki tatu au nne, utaona mabadiliko.
Vitu vingine vinavyoweza kusaidia kuondoa madoa, ni asali na siki (vinegar), ambapo matumizi yake, unapaka usoni na kusubiri mpaka dakika thelathini zipite.
Leo nimeamua kukuletea mbinu za asili za namna ya kuondoa kabisa madoa ya chunusi, kwa kutumia njia za asili. Wengi hutumia krimu kali na matokeo yake, hujichubua rangi za ngozi zao na husababisha matatizo makubwa zaidi.
Mahitaji
- Malimao au juisi ya malimao
- Maji safi
- Kitambaa safi cha pamba
Tengeneza juisi ya malimao bila kuongeza maji au kitu kingine chochote. Paka usoni na iache ikauke kabisa. Subiri mpaka baada ya dakika thelathini, osha uso wako. Unaweza kutumia pia kitambaa cha pamba kujisugua taratibu kwenye uso wako kisha nawa vizuri.
Unaweza kurudia zoezi hili hata mara mbili kwa siku na endelea mpaka wiki tatu au nne, utaona mabadiliko.
Vitu vingine vinavyoweza kusaidia kuondoa madoa, ni asali na siki (vinegar), ambapo matumizi yake, unapaka usoni na kusubiri mpaka dakika thelathini zipite.
ZeroDegree.
Tumia Juisi ya Limao kuondoa madoa ya chunusi usoni
Reviewed by Zero Degree
on
1/12/2017 01:35:00 PM
Rating: