Loading...

Wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo kuhusu njaa kuchukuliwa hatua

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameonya kuwa watu wakiwemo wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo za kuwepo kwa baa la njaa, ni kosa na wachukuliwe hatua ikiwemo kukamatwa.

Naibu waziri huyo alitoa onyo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya Jumatatu hii mkoani Rukwa ambako Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alimhakikishia kuwa mkoa huo hauna njaa, bali una ziada ya kutosha.

“Nyie wenyewe mmemsikia mkuu wa mkoa Zelothe amethibitisha kuwa hakuna njaa mkoani hapa lakini sio hapa tu, pia mikoa ya Mbeya na Songwe wamenithibitishia kuwa hawana njaa,”

Aliongeza “Sasa wapo wanasiasa uchwara wanaeneza propaganda kuna njaa, sio mamlaka yao kutangaza kuwa kuna njaa, kueneza uongo kama huo ni si sawa kwa kuwa kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini, wanastahili kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa”.

Siku chache kabla ya Naibu waziri huyo kufika katika mkoa humo, Zelothe alitoa taarifa kuhusu hali ya chakula mkoani kwake na alisema kuwa mkoa wake una chakula.

ZeroDegree.
Wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo kuhusu njaa kuchukuliwa hatua Wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo kuhusu njaa kuchukuliwa hatua Reviewed by Zero Degree on 1/24/2017 10:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.