Loading...

Afcon: Misri watinga fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mikwaju ya penati [Video]

Golikipa wa Misri Essam El-Hadary akiokoa moja ya penelti hizo
Golikipa mkongwe wa timu ya taifa ya Misri mwenye umri wa miaka 44, Essam El-Hadary ameokoa penalti mbili na kuiwezesha nchi hiyo kutinga fainali ya michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) inayoendelea nchini Gabon kwa kuitoa Burkina Faso kwa penelti 4-3.

Hadi muda wa nyongeza timu hizo zilikuwa sare ya goli 1-1 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Stade de l'Amitie, Libreville.

Wafunga wa magoli hayo katika muda wa dakika 90 walikuwa Mohamed Salah katika dakika 66 kwa upande wa Misri na Aristide Bance dakika 77 kwa upande wa Burkina Faso.

Leo ni nusu fainali ya pili kati ya Cameroon na Ghana.


Afcon: Misri watinga fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mikwaju ya penati [Video] Afcon: Misri watinga fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mikwaju ya penati [Video] Reviewed by Zero Degree on 2/02/2017 12:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.