Loading...

Haitakuwa rahisi kututoa kileleni mwa ligi, Haruna Niyonzima

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima.
KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa, kwa sasa hakuna wa kuwaondoa kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu.

Niyonzima, alisema kuwa, wanajiandaa kuendeleza dozi kwenye mchezo wao dhidi ya Stand United utakaochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.

"Muda mrefu tulikuwa tunafikiria kukaa kileleni, tumepata nafasi hiyo na kwa sasa haitakuwa rahisi kushuka, tunajipanga kuendeleza ushindi katika kila mchezo kuanzia huu dhidi ya Stand United," alisema Niyonzima.

Niyonzima, alisema wanaosubiria timu hiyo ishuke kileleni watasubiri kwa muda mrefu kwa kuwa lengo lao ni kutetea ubingwa wao.

Yanga itapambana na Stand jumapili wakiwa wametoka kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mwadui FC wiki iliyopita ushindi ambao umewapandisha mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

Kikosi hicho cha kocha George Lwandamina, kinaongoza kwa tofauti ya pointi moja ikiwa imekusanya pointi 46 huku Simba ikiwa na pointi 45 na kushika nafasi ya pili.
Haitakuwa rahisi kututoa kileleni mwa ligi, Haruna Niyonzima Haitakuwa rahisi kututoa kileleni mwa ligi, Haruna Niyonzima Reviewed by Zero Degree on 2/02/2017 12:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.