Alichosema Beckham juu ya tuhuma kuwa alitumia uhusiano wake na UNICEF kusaka cheo cha ‘SIR’ Uingereza
David Beckham amekanusha ripoti kuwa alitumia uhusiano wake na shirika la umoja wa mataifa, UNICEF kupigia kampeni cheo cha ‘Usir’ nchini Uingereza.
Ijumaa, gazeti la Uingereza, The Sun, lilichapisha barua pepe zilizovuja, kati ya staa huyo wa soka na msemaji wake mwaka 2013 ambapo walijadiliana kuhusu kutafuta cheo (knighthood).
Kwenye barua pepe hizo, Beckham, aliyetunukiwa Order of the British Empire mwaka 2003, aliiita tuzo hiyo aliyopewa muimbaji Katherine Jenkins kuwa ni utani “a f**king joke,” na kuielezea kamati inayoamua nani anastahili kupewa heshima hiyo “bunch of c**ts.”
Msemaji wake amedaiwa kumsihi Beckham kujikita kwenye shughuli za kujitolea kama ubalozi wa UNICEF, ambao amekuwa nao tangu mwaka 2005. Jumamosi, msemaji wake, alimtetea baba huyo wa watoto wanne kuwa ripoti hizi zimemtengenezea picha ya tofauti kwa makusudi.
“David Beckham na UNICEF wamekuwa na muungano wenye nguvu katika harakati za kusaidia watoto kwa miaka 15. Kampeni ya 'The David Beckham 7 Fund' imechangingia mamilioni ya paundi na kusaidia mamilioni ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu duniani,” yalisema maelezo yake.
“David Beckham ametoa uda wake na nguvu yake na vile vile kutumia pesa ya kwake binafsi katika suala zima la kuwasaidia watoto na moyo huo hautakuwa na kikomo utaendela mpaka mwisho.”
Nayo UNICEF, ilitoa maelezo yake na kupongeza kazi za Beckham na shirika hilo.
“David Beckham amekuwa ni balozi wetu mwenye nia nzuri tangu mwaka 2005, na mtu wa kutoa muda wake, nguvu yake na kutoa msaada katika kuasaidia kuongeza fedha kwa shirika la UNICEF kwa kazi yake ya kusaidia watoto, David amekuwa akitoa pesa yake binafsi,” maelezo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya UNICEF.

Reviewed by Zero Degree
on
2/06/2017 06:32:00 PM
Rating: