Loading...

Ujumbe wa winga wa Yanga, Simon Msuva kwa Simba SC

WINGA wa Yanga, Simon Msuva, amesema watani wao wa jadi Simba watajuta kuwapisha kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Msuva alisema moja ya kosa walilolifanya Simba ni kuwapisha kileleni baada ya kufungwa bao 1-0 na Azam.

Msuva alisema wataendelea kukaa keleleni baada ya kuwafunga katika mchezo wao utakaochezwa Februari 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

“Akili za wana-Simba ni kutaka kutufunga sisi, hili halitawezekana kutokana na malengo yetu ni kutetea ubingwa wetu.

Simba walishafanya kosa la kuturuhusu kukaa kileleni wasipokuwa makini watakuja kujuta tutapokutana Februari 25 kwani tunajipanga kuhakikisha tunawafunga,” alisema Msuva.

Msuva alisema kikosi chao kipo vizuri na kipana hivyo wanauhakika wa kuifunga Simba katika mchezo wao unaokuja.

Source: Bingwa
Ujumbe wa winga wa Yanga, Simon Msuva kwa Simba SC Ujumbe wa winga wa Yanga, Simon Msuva kwa Simba SC Reviewed by Zero Degree on 2/06/2017 06:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.