Loading...

Ancelotti aelezea sababu ya kuwaonesha mashabiki kidole cha kati

Baada ya kocha wa FC Bayern Munich ya Ujerumani Carlo Ancelotti kutakiwa kutoa maelezo ya kwanini alikosa uvumilivu na kuwatukana kwa kuwaonesha kidole cha kati mashabiki wa Hertha BSC wakati wa mchezo dhidi ya timu yake, ameamua kuweka wazi kwanini alifanya hivyo.

Katika mchezo huo ambao FC Bayern Munich walicheza ugenini, walinusurika na kipigo baada ya Robert Lewandowski kuisawazishia goli dakika ya 90, goli ambalo walifungwa toka dakika ya 20 na Vedad Ibisevic na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Utajiuliza ni sababu gani ilimfanya Ancelotti kuonyesha kidole cha kati? mwenyewe amekiri kufanya kitendo cha kuwaonesha kidole cha kati na kueleza kwa ufupi tu >>> “Ndio nilionesha ishara ya kidole cha kati kama ambavyo nilitemewa mate awali“
Ancelotti aelezea sababu ya kuwaonesha mashabiki kidole cha kati Ancelotti aelezea sababu ya kuwaonesha mashabiki kidole cha kati Reviewed by Zero Degree on 2/21/2017 04:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.