Loading...

VIDEO: Arsenal yakubali kichapo cha pili mfululizo, ..Leo ikiwa ni cha goli 3 - 1 toka kwa 'The Blues'

Chelsea wametoka kifua mbele katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal nakuongeza pointi 3 zaidi hadi kufikia pointi 9 na kuzidi kujikita kileleni wakati walipokuwa wakiikaribisha Arsenal iliyo nafasi ya tatu nyuma ya Tottenham wanaoshikilia nafasi ya pili ambao wanamchezo dhidi ya Middledlesbrough saa mbili na nusu usiku wa leo.

Chelsea wameibuka na ushindi wa goli 3-1, Magoli ya Chelsea yakifungwa na Marcos Alonso dakika ya 13, Eden Hazard dakika ya 53, Fabregas dakika ya 85, na goli pekee la Arsenal likifungwa na Giroud dakika za nyongeza.

Fabregas amefanikiwa kuipatia timu yake ya Chelsea goli la tatu na kuihakikishia ushindi katika mechi dhidi ya mahasimu wao. Fabregas alitokea benchi akichukua nafasi ya Eden Hazard na kufungu goli la tatu ikiwa ni dakika yake ya pili tu akiwa mchezoni.

Mechi hii kwa Chelsea ilikuwa ni fursa kujivua aibu baada ya kufungwa na arsenal goli tatu bila katika mechi ya awali.

Na baada ya kupoteza mchezo huo wa awali dhidi ya Arsenal, ikumbukwe kuwa ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa Chelsea kufululiza matokeo mazuri.

Arsenal ambao jumanne walipokea kichapao cha Watford, wameingia na wasiwasi mkubwa hasa baada ya kiungo wao Aron Ramsey kuumia mguu.

Pia wamezikosa huduma za Granit Xaka anayetumikia adhabu huku Mohamed Elneny akiwa michezo ya fainali za kombe la Afrika na timu yake ya Misri.

Michezo ya kesho Jumapili itakuwa ni kati ya Manchester City ambao watachuana na Swansea City huku Leicester City wakiikaribisha Man United


VIDEO: Arsenal yakubali kichapo cha pili mfululizo, ..Leo ikiwa ni cha goli 3 - 1 toka kwa 'The Blues' VIDEO: Arsenal yakubali kichapo cha pili mfululizo, ..Leo ikiwa ni cha goli 3 - 1 toka kwa 'The Blues' Reviewed by Zero Degree on 2/04/2017 06:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.