Loading...

Askari feki wamemtapeli mfanyabiashara toka Dar es Salaam

Mfanyabiashara mkazi wa jijini Dar es Salaam, Muheshi Kumar Peddy (25), amenyang’anywa shilingi 1,597,000 taslimu pamoja na simu mbili aina ya Galaxy na moja ya kawaida na watu wanne waliojitambulisha ni maafisa Polisi.

Watuhumiwa hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi,baada ya kujitambulisha kwa mfanyabiashara huyo, walidai kuwa wana mashine kwa ajili ya kukagua shilingi 90 milioni zilizoibwa siku za nyuma.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, ACP Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea januari 30 mwaka huu, saa 10.30 jioni katika nyumba ya kulala wageni iitwayo ATN iliyopo Manyoni mjini.

Alisema mfanyabiashara Muheshi aliweza kuwapeleka watuhumiwa hao kwenye chumba namba 202 na kuwaonyesha fedha hizo na simu hizo za kingajani.

“Baada yapo walimnyang’anya fedha hizo pamoja na simu hizo na kisha kuondoka kwa gari lao T.690 BCU aina ya Toyota crester nyeusi. Watu hao walielekea Dodoma kupitia barabara kuu ya lami,” alisema

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema askari polisi waliokuwa kwenye doria walipata taarifa hiyo na mara moja walianza kulifukuzia gari hilo na kufanikiwa kulikamata kwenye maeneo ya mlima Saranda.

Debora alisema Polisi hao waliweza kumkamta dereva wa gari hilo Amru Oden Mwafungo (37) mkazi wa Sayi – Mbeya.

“Baada ya kumkamata dereva Amru,polisi hao walifanya msako mkali na kufanikiwa kumkamta Frank Massawe (25) mkazi wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro akiwa na fedha zilizoibwa shilingi 1,597,000 na simu mbili za mlalamikaji Muheshi,” alisema.

Kamanda Debora alisema Frank alikamatwa akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitayo BRM chumba namba K1.Watuhumiwa wengine wawili, waliweza kukimbilia kusikojulikana.

Kamanda Magiligimba, ametoa wito kwa wananchi kujenga uthubutu wa kukataa kuhojiwa na watu wasiowafahamu na wale wanaojitambulisha kuwa ni maafisa wa Serikali au kutoka Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, Kamanda huo alisema kuwa dereva mkazi wa Kindai mjini Singida, Hassani Athumani Ntunda (44), amefariki dunia baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu.

Alisema dereva huyo amefariki dunia januari 30 mwaka huu saa 2.30 asubuhi huko katika kijiji cha Minyughe wilaya ya Ikungi,

Akifafanua, alisema dereva huyo alipewa chakula hicho na Hadija Soa (35) na kwamba mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
Askari feki wamemtapeli mfanyabiashara toka Dar es Salaam Askari feki wamemtapeli mfanyabiashara toka Dar es Salaam Reviewed by Zero Degree on 2/01/2017 01:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.