Loading...

Aubameyang mguu nje mguu ndani kuondaka klabu ya Dortmund

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang amefunguka mipango yake na klabu hiyo ya Ujerumani baada ya kuwepo tetesi nyingi ambazo zinamhusisha yeye kuhama na kwenda vilabu vingine vikubwa barani Ulaya.

Aubameyang amesema kuwa kwa sasa hajui ni nini mustakabali wa maisha yake kama ataondoka au atabakia Dortmund na kama kama hataondoka basi atamalizia muda wake wote wa soka akiwa katika klabu hiyo.

“Ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza sana, hasa kwa kipindi hiki kuhusu kuondoka, muda mwingine najisikia vizuri kuwepo hapa kutokana na uwepo na mashabiki wazuri. Ni klabu kubwa lakini najuliza swali mwenyewe kama nikitaka kupiga hatua, natakiwa kuondoka?,

“Sina jibu, itachukua muda kidogo. Nina miaka 27 kama ninataka kufanya jambo basi lipo linafanyiwa kazi, alafu tafanya maamuzi baada ya msimu kumalizika,” alisema Aubameyang na kuongeza.

“Nataka nione itakavyokuwa, kama nitaweza kucheza nitasalia hapa, na namaanisha tamaliza maisha yangu ya soka hapa, nitachukua muda kulitafakari hilo.”
Aubameyang mguu nje mguu ndani kuondaka klabu ya Dortmund Aubameyang mguu nje mguu ndani kuondaka klabu ya Dortmund Reviewed by Zero Degree on 2/01/2017 06:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.