Hii hapa sababu ya baadhi ya Wizara kutumia majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM]
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema chuo hicho kina majengo mengi ya ziada ambayo kwa sasa hayatumiki.
Waziri Mhagama ametoa ufafanuzi huo, bungeni mjini Dodoma mapema leo, baada ya Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Suzan Lyimo kuhoji sababu za Serikali kuhamishia ofisi zake na makazi katika baadhi ya majengo ya UDOM.
Katika swali hilo la nyongeza, Lyimo alitaka kujua ikiwa Serikali imekurupuka katika uamuzi wake wa kuhamishia ofisi zake katika mji huo uliopo katikati ya nchi ama la.

Waziri Mhagama ametaka wizara nyingine kufanya uamuzi wa kuhamia Dodoma na kutumia majengo ya UDOM kwani serikali ilijenga majengo mengi ambayo hayatumiki kwa sasa.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angellah Kairuki alihamia mjini Dodoma, ikiwa ni utekelezaji wa tamko la Rais John Magufuli la kuhamishia shughuli za serikali makao makuu ya nchi.
Hii hapa sababu ya baadhi ya Wizara kutumia majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM]
Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2017 06:30:00 PM
Rating: