Padri aiomba serikali kupiga marufuku pombe ya viroba
Serikali imeombwa kupiga marufuku pombe kali zinazohifadhiwa kwenye karatasi maarufu kama ‘viroba’ ili kuwanusuru vijana wengi wanaoathirika na kujiingiza katika ulevi wa pombe hizo.
Mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa na wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu mkoani Manyara, Padri James Amnaay ametoa wito huo Jumatano hii alipokabidhiwa msaada wa vyakula, nguo na sabuni na UWT, Mbulu katika maadhimisho ya miaka 40 ya CCM.
Padri Amnaay amesema endapo Serikali itapiga marufuku pombe hizo, vijana wengi hawatajiingiza kwenye ulevi huo unawasababisha wakithiri katika ulevi huo na kuwafanya wawe vichaa. Amesema kutokana na urahisi wa kubebwa na bei nafuu, pombe hizo za karatasi zimewaathiri vijana wengi wanaokunywa na kulewa kisha kujiingiza kwenye dawa za kulevya na kuwasababishia kuwa vichaa.

Source: Mwananchi
Padri aiomba serikali kupiga marufuku pombe ya viroba
Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2017 06:20:00 PM
Rating: