Loading...

CAG aagizwa kuchunguza mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania [ATCL]

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Asad.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Aliyasema hayo baada ya kutembelea Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam jana kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

“Nitamuagiza CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” alisema.

Waziri Mkuu alisema serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo aliwataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya taifa.

Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kielektroniki ili kuzuia upotevu wa mapato.

“Vitu vingi vinavyoenda `manual' ni rahisi kufa. Serikali tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu tumepata mafanikio,” alisema.

Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Witness Mbaga, ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.

Aidha, Majaliwa amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
CAG aagizwa kuchunguza mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania [ATCL] CAG aagizwa kuchunguza mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania [ATCL] Reviewed by Zero Degree on 2/10/2017 11:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.