Loading...

Orodha mpya ya FIFA ya viwango bora vya soka Duniani, ..Argentina bado vinara wakati Tanzania ikizidi kuporomoka

Shirikisho la soka Ulimwenguni (FIFA) hapo jana limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka Duniani kwa nchi Wanachama , na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika ni Misri ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.

5 Bora kwenye orodha hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Taarifa ya Fifa iliyotolewa leo inaonesha kuwa Tanzania imetoka nafasi ya 156 hadi 158 na kuendelea kuwa nyuma ya nchi nyingine wananchama wa CECAFA ikiwemo Uganda (75), Kenya (87), Rwanda (100) na Burundi (183). 

Mwanachama mpya wa Jumuiya ya Africa Mashariki Sudan Kusini inashilikia nafasi ya 169 katika msimamo huo ambao Argentina bado ni vinara wakifuatiwa na Brazil, Ujerumani, Chile, Ubelgiji, Ufaransa, Colombia, Ureno, Uruguay na Hispania.

Kwa upande mwingine mashindano ya AFCON yaliyomalizika hivi karibuni nchini Gabon yamezinufaisha baadhi ya nchi ikiwemo mabingwa wapya Cameroon waliopanda kwa nafasi 29 na kuwa nafasi ya 33 duniani huku makamu bingwa, Misri ikipanda hadi nafasi ya 23 huku ikiongoza kwa ubora barani Afrika.


Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Misri, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ni Cameroon, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.

Orodha hiyo ni;
  1. Argentina
  2. Brazil
  3. Germany
  4. Chile
  5. Belgium
  6. France
  7. Colombia
  8. Portugal
  9. Uruguay
  10. Spain
  11. Switzerland
  12. Wales
  13. England
  14. Poland
  15. Italy
  16. Croatia
  17. Mexico
  18. Peru
  19. Costa Rica
  20. Iceland
Kwa upande wa Afrika Mashariki Uganda bado wanaendelea kuongoza wakiwa nafasi ya 17 kwa Afrika na 75 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 20 Afrika na 87 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 27 Afrika na 100 duniani na Burundi nafasi ya 40 Afrika na 138 duniani

Kwa upande wa Afrika Misri wamekuwa vinara kwa kukwea kwa nafasi 12 na kutua kileleni wakiwa nafasi ya 23, wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 31 huku mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi 29 mpaka nafasi ya 33 duniani.
Orodha mpya ya FIFA ya viwango bora vya soka Duniani, ..Argentina bado vinara wakati Tanzania ikizidi kuporomoka Orodha mpya ya FIFA ya viwango bora vya soka Duniani, ..Argentina bado vinara wakati Tanzania ikizidi kuporomoka Reviewed by Zero Degree on 2/10/2017 11:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.