Loading...

Conte: Unapokuwa na wachezaji wa aina hii, utapata usingizi mzuri bila shaka

Kama anavyoendelea kupigania (Conte) nafasi ya Pedro kikosini, Willian kwa sasa amekuwa ni mtu wakuonekana ndani na wakati mwingine nje ya kikosi cha Conte.

Japokuwa 'The Blues' ilikuwa na msimu mbaya wa kukatisha tamaa mwaka jana, Willian alikuwa mchezaji wa klabu na kufanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo.

Licha ya nyota huyo (Willian) mwenye umri wa miaka 28 kutumia muda wake mwingi akiwa kwenye benchi wakati huu, bosi huyo wa Chelsea anasema ana wachezaji wenye ubora anaoutaka pale Stamford Bridge.


Muitaliano huyo pia alizungumzia sana mchango wa Cesc Fabregas kwa timu baada ya kuifungia bao la kuongoza katika mchezo wa Chelsea 3-1 dhidi ya Swansea siku ya Jumamosi.

"Yeye [Fabregas] alionyesha uwezo mkubwa wa kiutaalamu," Conte aliambia tovuti ya Chelsea.

"Ninafuraha kuwa na fursa kama hii ya kufanya kazi na aina ya wachezaji kama
 hawa.

"Tunazungumzia mabingwa, si wachezaji wenye uwezo wa kati, bali wachezaji wenye uwezo wa juu.

"Wakati unapokuwa na wachezaji kama hawa kikosini ambao huipa kipaumbele timu na sio kujifikiria wao wenyeyewe, lakini mawazo ni katika mafanikio ya  timu yao, ni jambo kubwa na lakufurahisha.

"Mfano mwingine ni Willian. Pedro amepata nafasi kubwa ya kucheza lakini tabia ya Willian iko sawa daima na wakati wowote unapokuwa na wachezaji wa aina hii, lazima uende katika nyumba yako kulala (vizuri). "
Conte: Unapokuwa na wachezaji wa aina hii, utapata usingizi mzuri bila shaka Conte: Unapokuwa na wachezaji wa aina hii, utapata usingizi mzuri bila shaka Reviewed by Zero Degree on 2/28/2017 02:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.