Loading...

Edward Lowassa kushuhudia mchezo wa Simba na Yanga leo

WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa leo atakuwa miongoni mwa maelfu ya mashabiki watakaohudhuria pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Lowassa, Aboubakar y Liongo, Lowassa ameamua kwenda kushuhudia mchezo huo kutokana na mapenzi yake kwenye soka.

"Kesho (leo) na kwenda Uwanjani.., usitake kujua mimi ni mshabiki wa timu gani, subiri utaniona uwanjani" alisema Lowassa kwenye taarifa yake hiyo.

Lowassa hajawahi kuweka wazi timu anayoishabikia hapa nchini lakini amewahi kukiri kwa upande wa timu za nje ni shabiki wa klabu ya Manchester United ya England.

Lowassa amesema kinachomsukuma zaidi kwenda uwanjani ni kuungana na wadau wa soka nchini kutaka kuiona ligi ya mpira Tanzania inakuwa na msisimko kama zilivyo ligi za nje.

"Nasikitika ninapoona watu tunazipenda sana timu za nje.., yale mahaba ya zamani kwa timu zetu yako wapi?michezo hususani mpira ni eneo pana sana la ajira kwa vijana wetu" alisema Lowassa.

Mchezo huo wa Simba na Yanga unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa soka nchini na utaanza saa 10:00 jioni.
Edward Lowassa kushuhudia mchezo wa Simba na Yanga leo Edward Lowassa kushuhudia mchezo wa Simba na Yanga leo Reviewed by Zero Degree on 2/25/2017 10:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.