Loading...

Frank Lampard atangaza kustaafu kucheza soka

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Chelsea, Frank Lampard amestaafu na kuhitimisha safari yake ya miaka 21 katika soka la ushindani.

Kwa mujibu wa BBC Sport, mkongwe huyo mwenye miaka 38 ambaye msimu uliopita aliitumikia New York City ya Marekani, ametangaza uamuzi huo kupitia mtandao wa kijamii.

 
Hadi anatangaza uamuzi huo, rekodi zinaonyesha kuwa Lampard amecheza mechi 649 akiwa na Chelsea.

“Pamoja na kupata idadi kubwa ya ofa za kucheza, lakini kwa umri huu wa miaka 38, ni vema nikaanza ukurasa mpya wa maisha yangu,” BBC Sport imemnukuu kiungo huyo.
Frank Lampard atangaza kustaafu kucheza soka Frank Lampard atangaza kustaafu kucheza soka Reviewed by Zero Degree on 2/03/2017 12:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.