Loading...

Goli la Mshambuliaji, Laudit Mavugo lilivoacha gumzo Songea

BAO la mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, dhidi ya Majimaji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi, limekuwa gumzo baada ya mchezaji huyo kumbetulia beki mpira uliompita kiunoni na kufunga kwa uhodari mkubwa.

Katika mchezo huo ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Mavugo alifunga bao hilo la tatu na kusababisha benchi la ufundi kulipuka kwa furaha na kwenda kujumuika naye kushangilia.

Baadhi ya watu wa benchi la ufundi walioonekana kujumuika na Mavugo ni pamoja na meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’, Mtunza vifaa wa timu, Hamis Mtambo na wachezaji wengine waliokuwa benchi kama mlinda mlango Manyika Peter.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mavugo alisema amefurahi kufunga bao hilo na anaamini ana uwezo mkubwa wa kucheza soka licha ya baadhi ya mashabiki kubeza kiwango chake.

Mavugo alisema ataendelea kusaka mabao ili kuhakikisha timu yake inachukua ubingwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba walipata bao la kuongoza kupitia kwa Ibrahim Ajib kabla ya Said Ndemla kuongeza la pili na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 48, ikishika nafasi ya pili nyuma ya Yanga waliowazidi pointi moja.
Goli la Mshambuliaji, Laudit Mavugo lilivoacha gumzo Songea Goli la Mshambuliaji, Laudit Mavugo lilivoacha gumzo Songea Reviewed by Zero Degree on 2/06/2017 11:07:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.