Loading...

Yanga kuvaana na 'Ngaya Club' ya Comoro katika Ligi ya mabingwa Afrika

Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kuondoka Ijumaa ijayo kwenda Comoro kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Ngaya Club.

Huu ni msimu wa pili mfululizo kwa klabu ya Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na inaanza na timu za Comoro baada ya mwaka jana pia kuitoa Cercle de Joachim kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani katika Raundi ya Awali.

Katika Raundi ya Kwanza Yanga iliitoa APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 ugenini na kutoa sare ya 1-1 nyumbani.

Mbio za Yanga katika Ligi ya Mabingwa ziliishia Raundi ya Pili inayohusisha timu 16, baada ya kutolewa na wababe wao wa kihistoria, Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2, ikitoa sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 Alexandria ndani ya dakika 120 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Yanga ikaangukia katika kinyanga'anyiro cha kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako iliitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 Dar es Salaam Mei 7 na kufungwa 1-0 Mei 18 katika mchezo wa marudiano Esperanca, Angola.

Katika mechi za makundi, Yanga ilishinda mchezo mmoja tu dhidi ya MO Bejaia ya Algeria Agosti 13, 2016 na kutoa sare moja na Medeama ya Ghana Julai 16, 2016 zote uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi nyingine ilifungwa 1-0 Bejaia Juni 20 ugenini, ikafungwa 1-0 nyumbani na TP Mazembe ya DRC Juni 28, ikafungwa 3-1 na Medeama Julai 26 ugenini kabla ya kumaliza kwakipigo cha 3-1 mbele ya Mazembe Agosti 23 mwaka jana Lubumbashi.
Yanga kuvaana na 'Ngaya Club' ya Comoro katika Ligi ya mabingwa Afrika Yanga kuvaana na 'Ngaya Club' ya Comoro katika Ligi ya mabingwa Afrika Reviewed by Zero Degree on 2/06/2017 11:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.