Loading...

Hii hapa Orodha ya washindi wa tuzo za AFCON 2017, ..Christian Bassong mchezaji bora

MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Christian Bassogog amekuwa Mwanasoka Bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka 2017.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ameisaidia sana Cameroon kutwaa Kombe la AFCON, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri kwenye fainali jana Uwanja wa l’Amitie mjini Libreville na akatajwa Mchezaji Bora wa Mashindano na Kamati ya Ufundi ya CAF na kikundi cha Watathmini.

ORODHA KAMILI YA WASHINDI AFCON 2017
  1. Mchezaji Bora wa Mashindano: Christian BASSOGOG (Cameroon)
  2. Mchezaji Bora wa fainali: Benjamin MOUKANDJO (Cameroon)
  3. Tuzo ya Fair Play: Misri
  4. Mfungaji Bora: Junior KABANANGA (DRC) Mabao 3
  5. Kikosi cha Mashindano cha CAF
    Kipa: Fabrice ONDOA (Cameroon)

    Mabeki: Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri), Michael NGADEU (Cameroon)

    Viungo: Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Misri)

    Washambuliaji: Christian BASSOGOG (Cameroon), Junior KABANANGA (DRC)
Hii hapa Orodha ya washindi wa tuzo za AFCON 2017, ..Christian Bassong mchezaji bora Hii hapa Orodha ya washindi wa tuzo za AFCON 2017, ..Christian Bassong mchezaji bora  Reviewed by Zero Degree on 2/06/2017 11:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.