Loading...

Kauli ya Kocha Pep Guardiola juu ya tetesi za Sergio Aguero kuondoka Manchester City

Uwezo ambao unaonyeshwa na kinda wa Manchester City, Gabriel Jesus ni wazi unatishia nafasi ya mshamhuliaji wa klabu hiyo, Sergio Aguero hali ambayo imezua maneno kuwa mchezaji huyo raia wa Argentina anaweza kuondoka.

Habari za ndani ya uongozi wa Man City zinasema kuwa klabu hiyo ya Uingereza bado inamuhitaji Aguero na hakuna mpango wowote kumwachia licha ya Guardiola kumwanzisha benchi katika michezo miwili mfululizo na nafasi yake ikichukuliwa na Jesus.

Aidha wiki iliyopita Aguero alinukuliwa akisema kuwa ana furaha kuwa sehemu ya wachezaji wa Manchester City na yeye binafsi hana mpango wowote wa kuondoka lakini uongozi ndiyo wenye uamuzi wa mwisho kama aondoke au abaki.

“Klabu ndiyo itaamua kuwa nina nafasi hapa au sina,” alisema Aguero ambaye ana mkataba na Man City hadi mwaka 2020.


Hata hivyo, kocha wa timu hiyo, Mhispania Pep Guardiola yeye amekuwa muwazi kabisa kuwa bado anahitaji kuwa na Aguero katika kikosi chake na ana mipango ya kumtumia kwa michezo ya mbeleni.

“Sergio atasalia kuwa moja ya wachezaji muhimu katika kikosi chetu na jambo ambalo tunataka kulifanya kwa kipindi kijacho, Sergio atakuwepo, ni muhimu iwe hivyo,” alisema Guardiola.
Kauli ya Kocha Pep Guardiola juu ya tetesi za Sergio Aguero kuondoka Manchester City Kauli ya Kocha Pep Guardiola juu ya tetesi za Sergio Aguero kuondoka Manchester City Reviewed by Zero Degree on 2/06/2017 11:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.