Loading...

Hizi hapa nchi 3 zenye idadi kubwa ya wakimbizi duniani, ..Sudan kusini ni mojawapo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeitaja nchi ya Sudan Kusini kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi.

Sudan Kusini imeshika nafasi hiyo, ikiwa nyuma ya Syria na Afghanistan ikiwa na wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni 1.5 na zaidi ya wananchi milioni 2.1 wa nchi hiyo wakiwa wamekimbia makazi yao.

UNHCR imesema kuwa kwa mwaka 2017 pekee, shirika hilo la wakimbizi linahitaji Dola milioni 782 (Trilioni 1.7 ya Kitanzania) kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi pekee wa Sudan Kusini.

Msemaji wa UNHCR, William Spindler alisema kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016 kulikuwa na wakimbizi 760,000 wa Sudan Kusini na nusu ya pili waliongezeka 500,000.

Aidha Spindler alisema asilimia 60 ya wakimbizi hao ni watoto na kwa mwaka 2017 wanategemea idadi ya wakimbizi kuongezeka kwani bado hakuna juhudi za uhakika zinazofanyika kurudisha hali ya usalama wa uhakika kuwa kama jinsi ilivyokuwa awali.

Kwasasa Sudan Kusini ina wanajeshi 13,500 wa Umoja wa Mataifa (UN) ambao wanalinda amani na UN mwezi Januari ilitaka kuongeza wanajeshi 4,000 lakini serikali ilikataa.
Hizi hapa nchi 3 zenye idadi kubwa ya wakimbizi duniani, ..Sudan kusini ni mojawapo Hizi hapa nchi 3 zenye idadi kubwa ya wakimbizi duniani, ..Sudan kusini ni mojawapo Reviewed by Zero Degree on 2/12/2017 12:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.