Loading...

Huu ndio mtazamo wa Ronaldinho juu ya kiwango cha mshambualiaji wa Manchester City, Gabriel Jesus

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Ronaldinho amemtaja mshambualiaji wa Manchester City, Gabriel Jesus kuwa kutokana na uwezo wake wa soka na umri wake basi ni wazi atafika katika kiwango cha Messi na Ronaldo na hata kuwa mchezaji bora wa dunia.

Ronaldinho amesema Jesus ana uwezo mkubwa na anaamini kiwango chake kitawatesa sana wapinzani wa Manchester City katika mashindano mbalimbali ambayo wanashiriki.



“Manchester City wana mchezaji mzuri sana Gabriel Jesus, na labda kwa baadae anaweza kuwa mchezaji bora wa dunia,” alisema Ronaldinho na kuongeza.

“Ukimwangalia Gabriel Jesus na hana hofu kabisa, anachotaka yeye ni kucheza na kuonyesha uwezo alionao, atawapa changamoto kubwa Manchester United, Liverpool, Chelsea na timu zingine kubwa kutokana na kiwango chake.”

Jesus mwenye miaka 19, mpaka sasa ameichezea timu ya taifa ya Brazil michezo sita na kufunga magoli matano na kwa upande wa Man City amecheza michezo miwili ya Ligi Kuu ya Uingereza na kufunga magoli mawili.
Huu ndio mtazamo wa Ronaldinho juu ya kiwango cha mshambualiaji wa Manchester City, Gabriel Jesus Huu ndio mtazamo wa Ronaldinho juu ya kiwango cha mshambualiaji wa Manchester City, Gabriel Jesus Reviewed by Zero Degree on 2/13/2017 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.