Kauli ya Rais Magufuli juu ya watanzania walioko magerezani ugaibuni kwa makosa ya 'unga'
RAIS John Magufuli amesema serikali haitajishughulisha na Watanzania waliokamatwa ughaibuni na kuhukumiwa kunyongwa kutokana na kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Huku akianika orodha mpya yenye maelfu ya Watanzania walio kwenye magereza ya ughaibuni tofauti na iliyotajwa Ijumaa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Magufuli alisema hukumu dhidi yao zinapaswa kutekelezwa na Tanzania haitahusika kuwatetea.
Rais Magufuli alituma 'salamu' hizo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Dk. Anna Peter na mabalozi watatu.
Rais aliwataka mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi mbalimbali kutojihusisha kwa vyovyote na wafungwa wa makosa ya madawa ya kulevya.
"Watanzania waliohukumiwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya, mabalozi msijihusishe nao... waacheni," Rais Magufuli alisema.
Rais Magufuli alituma 'salamu' hizo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Dk. Anna Peter na mabalozi watatu.
Rais aliwataka mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi mbalimbali kutojihusisha kwa vyovyote na wafungwa wa makosa ya madawa ya kulevya.
"Watanzania waliohukumiwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya, mabalozi msijihusishe nao... waacheni," Rais Magufuli alisema.
Kauli ya Rais Magufuli juu ya watanzania walioko magerezani ugaibuni kwa makosa ya 'unga'
Reviewed by Zero Degree
on
2/13/2017 12:37:00 PM
Rating: