Basi la City Boy lagongana na Fuso mkoani Tabora, 12 wafariki, 46 wajeruhiwa
Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Tabora, Insp Hardson, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni tairi la kulia la Fuso lilikutumbukia kwenye mashimo mawili na kusababisha tairi kupasuka na rimu kupinda hivyo likakosa mwelekeo na kuligonga basi la City Boy uso kwa uso.
Soma na hizi:
Insp Hardson amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya igunga huku baadhi ya majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Nkinga na wengine Bugando Mwanza kwa ajili ya matibabu.
TAARIFA YA AWALI YA AJALI YA CITY BOY NA FUSO KUTOKA TRAFFIC TABORA.
Nimefika eneo la tukio SAA 23:30hrs toka Tabora mjini 200Kms. Eneo ni Makomero tarafa na wilaya Igunga mkoa wa Tabora.
Gari T486 ARB aina ya FUSO likiwa na mzigo wa viazi ikitokea Singida kuelekea Igunga tairi ya kulia limetumbukia katika mashimo mawili barabarani kisha kupasua tairi na rim kupinda na mfumo wa usukani kukatika maungio ya steering rod na steering box kisha gari kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya City boy.
Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha, 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya Igunga.
Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya Wilaya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi ambapo wanaume wawili wamepelekwa Bugando Mwanza na mwanamke mmoja amepelekwa Nkinga usiku huu.
Dereva wa basi amefariki papo hapo. Wahusika wa FUSO kwa taarifa za awali inasemekana wamekimbia baada ya ajali hii.
Toka kwa Insp Hardson, Kaimu RTO Tabora.
Dereva wa basi amefariki papo hapo. Wahusika wa FUSO kwa taarifa za awali inasemekana wamekimbia baada ya ajali hii.
Toka kwa Insp Hardson, Kaimu RTO Tabora.
Basi la City Boy lagongana na Fuso mkoani Tabora, 12 wafariki, 46 wajeruhiwa
Reviewed by Zero Degree
on
4/05/2018 10:20:00 AM
Rating: