Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 5 Aprili, 2018

Antoine Griezmann
Baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Real Madrid, Juventus wamegundua kuwa mabadiliko makubwa ya kikosi chao yanahitajika ili kupata mafanikio kwenye michuano ya Ulaya. Na jina la kwanza kwenye orodha yao ni la nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann.

Mwenyekita wa klabu ya Napoli, Aurelio de Laurentiis anataka kumpa mkataba mpya Maurizio Sarri utakaoisha mwaka 2021 na kuongeza mshahara wake mara mbili. Anahofia kocha huyo anaweza kuondoka baada ya Monaco kuonyesha nia ya kumhitaji. (Corriere dello Sport)
 
Kiungo wa klabu ya Monaco, Fabinho anatarajiwa kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester United kwenye majira ya joto.

Jose Mourinho anataka Juan Mata aondoke katika kikosi cha  Manchester United na nyota wa Chelsea, Willian achukue nafasi yake.

Fulham wanatarajiwa kupokea kiasi cha pauni milioni 20 kwa kujaribu kumuuza kiungo wa klabu yao, Tom Cairney kwenda Newcastle.

Meneja wa West ham, David Moyes alimchunguza golikipa wa Fulham, Marcus Bettinelli kwenye mchezo wao dhidi ya Leeds Jumanne.

Everton na Bournemouth zitachuana vikali kwenye mbio za kuwania saini ya raia wa Misri, Mahmoud Hassan.

Sunderland, Birmingham na Hull ziko kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa klabu ya Doncaster, Niall Mason. (Sun)

Nyota anayewindwa na klabu ya Arsenal na Juventus, Max Meyer anawindwa pia na klabu za Ligi Kuu ya Ujerumani, Hoffenheim na RB Leipzg. Kiungo huyo wa Shalke 04 anamaliza mkataba wake kwenye majira ya joto. (Bild)

Licha ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Borussi Dortmund, golikipwa Paris Saint-Germain, Kevin Trapp anaweza asijiunge na klabu hiyo ya Ujerumani kwenye majira ya joto. (Kicker)
 
Carlos Carvalhal
Swansea wamefanya mazungumzo na Carlos Carvalhal juu ya kuongeza mkataba wake katika klabu hiyo hadi msimu ujao.

Real Betis ina hamu ya kumrejesha golikipa wa klabu ya West Ham, Adrian katika klabu yao kwenye majira ya joto.

Mchezaji aliyeitumikia Chelsea kwa muda mreru - Matej Delac - ataondoka katika klabu hiyo kwenda AC Horsens ya Denmark kwenye majira ya joto baada ya miaka tisa ya kuitumikia klabu hiyo ya Uingereza ambapo golikipa huyo alishindwa kuonekana kwenye kikosi cha kwanza. (Star)

Mwenyekiti msaidizi wa Southampton, Les Reed anakaribia kuchukua nafasi nyingine kama mkurugenzi mpya wa ufundi wa EPL. (Times)

Fulham watajaribu kumbakihsa meneja wao, Slavisa Jokanovic kwa kumpa mkataba mpya wenye mafao mazuri.

Southampton watajaribu kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Paco Alcacer kama watafanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne amesema kuwa alimpigia kula Mohamed Salah kwenye tuzo za mwaka za Mchezaji bora wa PFA.

Javier Hernandez anajiandaa kufikiri juu ya hatima yake katika klabu ya West Ham kwenye majira ya joto.

Meneja wa St Mirren, Jack Ross ni mgombea wa nafasi ya meneja wa klabu ya Charlton msimu ujao.

Sunderland, Sheffield United na Leeds ni miongoni mwa vilabu vinavyohitaji saini ya kiungo wa klabu ya Shrewsbury, Jon Nolan. (Mirror)

Massimiliano Allegri
Chelsea wameendeleza nia yao ya kumfanya Massimiliano Allegri kuwa meneja wao mpya.

Zlatan Ibrahimovic alikataa ofa ya karibu pauni milioni 70 kwa mwaka kutoka klabu ya Ligi Kuu ya China akachagua kuichezea LA Galaxy. (Daily Mail)

Tamaa ya Mousa Dembele ya mkataba mpya wa miaka mitatu inaweza kuwa chanzo cha mazungmzo ya kusalia Tottenham.

Arsene Wenger anafikiria kuvunja kiapo chake kwa David Ospina na kumuita Petr Cech kwenye mchezo wa Arsenal dhidi ya CSKA Moscow. (Telegraph)

Hatima ya Gareth Bale katika klabu ya Real Madrid iko shakani baada ya nyota huyo kukosa nafasi ya kushiriki mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.

Golikipa wa Sevilla, Sergio Rico anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Uhispania kwenye majira ya joto baada ya kuwekwa benchi kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus Jumanne. (AS)

Andreas Pereira
Kiungo wa Manchester United, ambaye anaichezea klabu ya Valencia kwa mkopo, Andreas Pereira anataka kufanya mazungumzo na meneja wake, Jose Mourinho kabla ya kuamua hatima yake katika dimba la Old Trafford. (ESPN)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 5 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 5 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/05/2018 11:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.