Loading...

Huyu ndiye mrithi wa Jenerali Davis Mwamunyange

Jenerali Venance Mabeyo
Rais John Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Taarifa hiyo imesema pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.
Huyu ndiye mrithi wa Jenerali Davis Mwamunyange Huyu ndiye mrithi wa Jenerali Davis Mwamunyange Reviewed by Zero Degree on 2/03/2017 11:21:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.