Loading...

Ibrahimovic awapa matumaini ya ubingwa mashabiki wa Manchester United

Baada ya kuifungia hat-trick Manchester United katika mchezo wa Ligi ya Vilabu Barani Ulaya dhidi ya Saint-Etienne, mshambuliaji wa klabu hiyo, Zlatan Ibrahimovic amesema sasa ni wakati wa kikosi cha timu hiyo kupata mafanikio.

Ibrahimovic amesema kwa sasa wana furaha na matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata na kwa idadi ya mashindano ambayo wanashiriki wanaamini lazima kuna makombe watashinda kama sio la Ligi Kuu ya Uingereza.

“Tuna furaha kwa sasa. Huu ni muda wa kufanya maamuzi kwa msimu huu na raundi ya pili ya msimu maamuzi ndiyo huwa yanafanyika,” alisema Ibrahimovic na kuongeza.

“Hayo ndiyo malengo yetu, bado tupo katika mashindano manne. Kama hatutashinda Ligi Kuu [Uingereza] basi tutashinda mataji mengine na hata hayo ni mazuri pia.”

Akizungumza kuhusu mchezo wa St Etienne, Ibrahimovic alisema, ”Kila ninapocheza dhidi ya Saint-Etienne nikijituma huwa ninafunga magoli mengi, na nimewafunga tena magoli mengi na ninatumaini ninaweza kufanya tena hivyo wiki ijayo.”
Ibrahimovic awapa matumaini ya ubingwa mashabiki wa Manchester United Ibrahimovic awapa matumaini ya ubingwa mashabiki wa Manchester United Reviewed by Zero Degree on 2/17/2017 12:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.