Loading...

TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Godfrey Bonny afariki dunia

Kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny maarufu kama Ndanje amefariki dunia katika Hospitali ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa nahodha wakati Bonny akiichezea Yanga, amethibitisha taarifa hizo.

Godfrey Bonny ‘Ndanje’ (wa pili kulia) akiwa na wachezaji wenzake
“Kweli nimepokea taarifa hizi za masikitiko, ndugu yetu ametangulia mbele za haki. Juhudi zilifanyika lakini Mungu alishapanga,” alisema Nsajigwa.


Mchezaji wa Yanga, Godfrey Bonny ‘Ndanje’ enzi za uhai wake

Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Prisons ya Mbeya. Baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Nepal ambako alicheza soka la kulipwa akiwa na Watanzania wengine akiwemo Nsajigwa.
TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Godfrey Bonny afariki dunia TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Godfrey Bonny afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 2/17/2017 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.