Loading...

Kaburi lililokutwa kwenye chanzo cha maji mkoani Arusha lazua utata

Kaburi lililokutwa kwenye chanzo cha maji cha Mto Nduruma wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha, limezua utata baada ya Serikali ya kijiji kwa kushirikiana na familia kutakiwa kufukua mwili na kuuhamisha.

Hatua hiyo inatokana na Mtendaji wa Kata ya Ambureni, Ayoub Meshili kuongoza wananchi kuharibu mazao yaliyooteshwa ndani ya hifadhi ya chanzo hicho cha maji.

Katika operesheni hiyo, kaburi la marehemu Jackson Simon (58), lilikutwa likiwa pembezoni mwa mto ndani ya hifadhi ya chanzo cha maji, hali iliyomfanya mtendaji huyo kuagiza Serikali ya kijiji kwa kushirikiana na familia kulihamisha.

Paulina (50), ambaye ni mjane wa marehemu Simon alisema waliamua kumzika eneo hilo kutekeleza wasia wake wa kuzikwa chini ya mti wa parachichi hivyo eneo hilo ndilo lilikuwa sahihi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Shangarai, Wilfred Kimaroi alisema atalishughulikia suala hilo kwa kukaa na familia ili kujua mahali salama na sahihi pa kuhamishia kaburi hilo.

Source: Mwananchi
Kaburi lililokutwa kwenye chanzo cha maji mkoani Arusha lazua utata Kaburi lililokutwa kwenye chanzo cha maji mkoani Arusha lazua utata Reviewed by Zero Degree on 2/08/2017 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.