Loading...

Rais wa TFF, Jamali Malinzi akanusha tuhuma za ufisadi

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinzi, amekanusha taarifa za uzushi zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amejichotea Sh bilioni moja bila baraka za Kamati ya Utendaji.

Malinzi amewaambia waandishi wa habari jijini kwamba, hakuna kitu kama hicho na yuko tayari kumwagiza Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, aongozane na vyombo vya habari ili kujionea miamala ya akaunti za Shirikisho hilo kama pesa zimechotwa.

“Niko tayari muondoke na Katibu akawahakikishie kama kuna hicho kiasi cha fedha kimetolewa, nadhani ni kundi la watu limeamua kufanya uzushi wenye lengo la kuichafua TFF kuelekea mbio za uchaguzi mkuu,” alisema.

Alisema hata fedha zenyewe zinazoelezwa kuchotwa kutoka katika mgao wanaopewa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) hazikutoka mwaka jana na wanatarajia kuzipokea hivi karibuni na kutaka wadau wa michezo kupuuza uzushi huo.

Source: Dimba
Rais wa TFF, Jamali Malinzi akanusha tuhuma za ufisadi Rais wa TFF, Jamali Malinzi akanusha tuhuma za ufisadi Reviewed by Zero Degree on 2/08/2017 01:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.