Loading...

Kufuatia tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, IGP awasimamisha kazi askari polisi 12

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 wa jeshi hilo ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma za kuhusika na mtandao wa biashara ya dawa za kulevya zinazowakabili.

Waliosimamishwa kwa tuhuma hizo ni SACP Christopher Fuime, Inspekta Jacob Hashim Swai, Sajenti Steven Ndasha, Sajenti Steven Shaga, Sajenti Mohamed Haima, Koplo Dotto Mwandambo, Koplo Tausen Mwambalangani, Koplo Benatus Luhaza, Koplo James Salala, Koplo Noel Mwalukuta, D/C Gloria Massawe na D/C Fadhili Mazengo.

Hatua hiyo, imekuja siku mbili baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutangaza majina ya askari na wasanii wanaohitajika kwenda kuhojiwa na jeshi la polisi, Kituo Kikuu, kwa madai ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Mbali ya kuwasimamisha kazi, IGP Ernest Mangu ameagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya askari waliotajwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Kufuatia tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, IGP awasimamisha kazi askari polisi 12 Kufuatia tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, IGP awasimamisha kazi askari polisi 12 Reviewed by Zero Degree on 2/04/2017 02:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.