Loading...

Kwa mara ya kwanza, ..Antonio Conte afunguka haya juu ya kiungo Cesc Fabregas

ANTONIO Conte amempongeza Cesc Fabregas kama 'mchezaji bora' na mwenye akili ya mpira wa miguu ya kuzaliwa nayo.
Baada ya muda mrefu wa kuanzia benchi kwa nafasi yake kujazwa na Kante pamoja na Nemanja Matic katika nafasi ya kiungo, Fabregas amepata wakati mgumu sana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya utawala wa Conte.

Mhispania huyo alijikuta hadi anahusishwa na hatua ya kuuzwa kwa mkopo na kuuzwa jumla kwa klabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na West Ham United na Manchester City.

Pamoja na yote hayo, bado heshima ya Antonio Conte kwa mkongwe huyo raia wa Spain, Cesc Fabregas.


"Cesc ni mchezaji bora wa hali ya juu na ni mwenye akili ya mpira wa miguu. Naweza kumzungumzia [juu yake] sawa na kama ningevyoweza kumzungumzia Andrea Pirlo. Kwa njia hiyo hiyo. Ndivyo tunavoweza kumzungumza mtu mwenye akili ya mpira wa miguu.

"Cesc kama yeye hana uwezo wa kukimbia mbio za mita 100 katika sekunde 10, naweza kumpa sifa hii, kwa sababu yeye ni mtaalamu na mpira. kasi yake iko katika akili yake. Kwa sasa, mimi pamoja na Cesc tunafanyia kazi mengi juu ya masuala kiufundi na kuboresha pia jinsi anavojiweka katka nafasi yake uwanjani. Kwangu mimi, nadhani Cesc ni mchezaji wa tofauti. " Hizo ni baadhi sifa za juu sana kutoka kwa muitaliano huyo.

Chelsea inaendelea kubaki juu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza [EPL], ikiwa mbele kwa pointi 10 zaidi ya klabu za London Arsenal na Tottenham Hotspur.
Kwa mara ya kwanza, ..Antonio Conte afunguka haya juu ya kiungo Cesc Fabregas Kwa mara ya kwanza, ..Antonio Conte afunguka haya juu ya kiungo Cesc Fabregas Reviewed by Zero Degree on 2/13/2017 04:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.