Loading...

Serikali imepiga marufuku kutumika kwa wimbo wa taifa katika mikutano ya vyama vya siasa

Ofisi ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali imeendelea kuikumbusha jamii pamoja na ofisi za umma, kuheshimu vielelezo vya Taifa na Nyaraka za serikali ikiwemo matumizi sahihi na halali ya Nembo, Wimbo na Bendera ya Taifa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Februari 13, 2017, Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo amepiga marufuku wimbo wa Taifa kupigwa katika sehemu zisizo rasmi ikiwemo vilabuni, sehemu za ibada na katika mikutano ya vyama vya siasa.

Aidha, ametoa maagizo kwa ofisi za umma zisizokuwa na bendera ya taifa kuwa nayo na kwamba ofisi itakayo kaidi agizo hilo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Kila ofisi ya serikali inatakiwa kuwa na bendera ya Taifa, Ofisi kadhaa hazitekelezi hilo, baadhi ya halmashauri hazitekelezi hilo. Unaogopa nini? Kama hutaki kuitambulisha ofisi yako kuwa ni ya serikali achia ngazi,” amesema.

Ameongeza kuwa “Bendera ya Taifa hairuhusiwi kuwekwa katika maeneo ya biashara, itumike mahali sahihi, pia marufuku kubandikwa iliyochakaa, pauka, au kutoboka atakaetumia hizo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini au kifungo cha miaka miwili jela.”

Katika hatua nyingine, Chibogoyo amesema ofisi yake imeandaa mikakati mipya ili kutokomeza uchapishaji wa nyara bandia. Pia amewataka wamiliki wenye viwanda vya kuchapisha nyara na wachapishaji kujiorodhesha ofisini kwake ili watambulike.

“Vita dhidi ya wachapishaji wa nyaraka bandia imekuwa ya mafanikio makubwa ingawaje wapo wasiotaka kuacha. Ofisi yangu itafuata nyayo kama walivyofanya Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, tutakua na msako wa nyumba kwa nyumba kwa kampuni zinazojihusisha na uchapishaji,” amesema.
Serikali imepiga marufuku kutumika kwa wimbo wa taifa katika mikutano ya vyama vya siasa Serikali imepiga marufuku kutumika kwa wimbo wa taifa katika mikutano ya vyama vya siasa Reviewed by Zero Degree on 2/13/2017 04:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.