Lissu, Mrema warushiana maneno kisa vita ya kuzuia dawa za kulevya
MWENYEKITI wa Parole, Augustino Mrema amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuwa anafanya makosa makubwa kutetea watuhumiwa wa dawa za kulevya.
Akizunguma na waandishi wa habari kwa simu jana, Mrema alisema anamshangaa Lissu kuwatetea watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kumshauri atumie elimu yake ya sheria kuwatetea waathirika na wanaotaja wahusika wa dawa za kulevya akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mbali na Lissu, Mrema aliigeukia mahakama itambue kuwa pamoja na kutafsiri sheria, jukumu la kuzuia dawa za kulevya lipo mikononi mwao.
“Nashangazwa na hawa wanaotuhumiwa kukataa kwenda kupimwa na kuonyesha juhudi za kuzuia zoezi hilo, wakubali kwenda kupimwa kwani ndio itakuwa kusafishwa kwao kama majibu yatatoka kuwa hawatumii,” alisema Mrema.
Akizungumzia kauli hiyo, Lissu alisema Mrema anapaswa kujiuzulu cheo alichopewa cha Mwenyekiti wa Parole kwa sababu alipewa kinyume cha sheria.
Alisema sheria ipo wazi kwamba Mwenyekiti wa Parole awe jaji au alishawahi kuwa jaji na si mwanasiasa kama Mrema.
“Ninapoona Mrema anapiga kelele, anatetea chakula chake na si vinginevyo, kisheria Mwenyekiti wa Palore anapaswa kuwa jaji au alishawahi kuwa jaji,”alisema Lissu.
Aidha kuhusu kuwatetea watuhumiwa, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema sheria ipo wazi kwamba wanachofanya mawakili kwa sasa ni kuwatetea watuhumiwa wote hata wanaotuhumiwa na dawa za kulevya, kwani sheria inamtaka wakili kutetea yeyote bila ubaguzi.

Source: Mtanzania
Lissu, Mrema warushiana maneno kisa vita ya kuzuia dawa za kulevya
Reviewed by Zero Degree
on
2/23/2017 11:38:00 AM
Rating: