Makaburi yageuka dili Jijini Dar
Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam ambayo katikati ya kaburi na kaburi huachwa nafasi kwa ajili ya ndugu kuja kuzika siku za baadaye. |
Wahenga walisema kufa kufaana. Usemi huu unatumiwa kikamilifu na baadhi ya wahudumu wa makaburi ambao kwao, uhaba wa maeneo ya maziko jijini Dar umekuwa fursa nzuri ya kujipatia kipato.
Jana, mwandishi mmoja wa gazeti la humu nchini alitembelea maeneo mbalimbali ya makaburi na kubaini kuwa baadhi ya wahudumu hao huuza hadi Sh300,000 kiwanja cha kaburi moja.
Mmoja ya watoa huduma hizo katika makaburi ya Buguruni Malapa, ambaye aliomba asitajwe alisema makaburi hayo yaliyo chini ya Kanisa la Anglikana, yamekuwa yakitumiwa kuzika wafu wa madhehebu tofauti kwa makubaliano na wahudumu hao.
“Hapa kwa dhehebu lako la Roma (alilojitambulisha mwandishi) unaweza kupata eneo ila itabidi utoe Sh300,000 tukufanyie utaratibu, kwa sababu hapa huwezi kupata eneo kwa urahisi,” alisema.
Katika makaburi ya Kisutu, mwandishi wetu alielezwa kuwa kuna makaburi ya familia ambayo marehemu mwingine hawezi kuzikwa.
Mhudumu wa makaburi hayo, Salehe Mwinyijuma alisema kuna maeneo katika makaburi hayo ila utaratibu huo wa kuyahodhi unalifanya ili kuonekana eneo hilo limejaa.
“Maeneo yapo kwa ndani ila wananchi wakija wanaweza kuona kama kumejaa. Huu utaratibu wa kuweka ndugu pamoja unasababisha watu waone kama kumejaa,” alisema Mwinyijuma.

Source: Mwananchi
Makaburi yageuka dili Jijini Dar
Reviewed by Zero Degree
on
2/21/2017 04:45:00 PM
Rating: